Wednesday, February 22, 2012

JUMATANO YA MAJIVU (ASH WEDNESDAY)


Maana yake na Umuhimu wake!
Ili kuelewa vizuri maana na umuhimu wa kipindi hiki, tutazame kwa ufupi haya yafuatayo: 

Sala ya mwanzo:
“Ee Bwana utujalie sisi waamini wako tuanze vita vya roho kwa mfungo Mtakatifu. Nasi tulio tayari kupigana na pepo wabaya, tujipatie nguvu kwasababu ya kufunga…”

Mahubiri:                   Padre Victor Tumaini akifafanua maana ya Kwaresma
Padre alifafanua kuwa...
“ ‘Majivu’ tunayopakwa siku ya leo ni ishara ya kufanya toba, ni ishara ya kumrudia Mungu! Tukitazama kwa ufupi baadhi ya vifungu katika Biblia tunaona ukweli huu:
-         Jer 6:26
-         Daniel 9:3
-         Yona 3:6
-         1Wamakabayo 3:46, ambapo Mathatia pamoja na wenzake walijipaka majivu kichwani kabla ya kuanza vita dhidi ya ukoloni. Ilikiwa ishara ya kumrudia Mungu ili awe nguvu ao katika mapambano waliokusudia kuyaanza dhidi ya ukoloni/ukandamizaji waliokuwemo!
-         Mt 10:13, Kristu naye alijua utamaduni huu wa toba wa kujipaka majivu pale alipoionya Korazin na Betsaida!
Mapokeo ya Kanisa Katoliki yameendeleza utamaduni huu wa toba:
-         Mnamo Karne ya 6 hadi ya 11 utamaduni huu ulifanyika, hata karne ya 12, papa Urbano wa Pili aliidhinisha majivu yatumike yale yatokanayo na matawi ya mizeituni yaliyotumika katika Jumapili ya Matawi.
Nabii Yoeli katika somo la kwanza (Yoe 2:12-18) anasistiza turarue mioyo wala si mavazi yetu…yaani, tufanye mabadiliko ya ndani na siyo ya nje tu!, kwa maneno mengine, mapinduzi ya kweli yaanze na yatoke mioyoni mwetu na si maonyesho ya njenje tu!
Injili ya leo (Mt 6:1-6, 16-18) iametuasa juu ya suala hilohilo la kufanya mfungo wenye msukumo wa kiroho unaotoka ndani ya moyo wa toba wa mtu na si kufanya kama Mafarisayo walivyokuwa wakifanya. Wao walifunga na kusali ili watazamwe na watu.
Tunapoanza kipindi cha Kwaresma kwa kupakwa majivu siku hii ya leo, tukumbuke wajibu wetu; -kufunga
-         Kusali zaidi na
-         kutenda matendo mema (matendo ya huruma) kwa jirani zetu!

Basi, tumuombe Kristu ili zoezi hili la mfungo wa Kwaresma lisiwe tukio la historian a la kupita tu, bali lizae matunda ya kiroho ndani mwetu, tufanye mapinduzi ya kweli ya kiroho na hatimaye atustahilishe kushiriki utukufu wake!”
Padre Tumaini akimpaka majivu Baba Rector
Frt P. Libongi mara baada ya kupakwa majivu(picha-juu)&Frt E. Mwita akipakwa majivu (picha-chini)
 


Sala ya kuombea Dhabihu:...Sala hii nayo hutukumbusha dhamira kuu ya adhimisho la leo.
“Ee Bwana tunatoa sadaka hii ya kuanza Kwaresma na kukuomba tuzishinde tamaa mbaya kwa matendo ya kitubio na mapendo. Nasi tukishatakaswa dhambi, tuwe na ibada ya kuadhimisha mateso yake mwanao…”

1 comment:

  1. Ahsante sana kwa kazi nzuri iliyofanyika!

    ReplyDelete